Rais Samia ataja sababu sita kwanini wawekezaji waichague Tanzania

0
13

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu sita za wafanyabiashara wa Oman kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa inatoa fursa za pekee za uwekezaji.

Akizungumza katika kongamano la biashara baina ya Omana na Tanzania mjini Muscat, amesema Serikali yake inajipanga kwa utekelezaji wa kuwezesha uwekezaji kwa urahisi.

Aidha, mambo aliyoyataja ni pamoja na amani, utulivu, utawala bora na mazingira mazuri, sera thabiti za uchumi na fedha, upatikanaji wa soko katika bara la Afrika, uwepo wa wafanyakazi wenye ujuzi, uwepo wa njia rahisi na za haraka pamoja na uhusiano wa kihistoria wa kindugu.

Amesema kuongezeka kwa uwekezaji kumeinufaisha Tanzania ambapo hadi kufikia Aprili 2022, ilisajili miradi 62 ya uwekezaji kutoka Oman yenye thamani ya dola za Marekani milioni 308.35 (sawa na zaidi ya TZS bilioni 717) pamoja na kutoa ajira 2,489.

Rais Samia amebainisha kuwa, biashara na uwekezaji wa nchi hizo mbili umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, lakini jitihada zaidi zinahitajika katika kuweka usawa wa kibiashara.

Raia kutoka Oman wamewekeza Tanzania katika sekta za kilimo, ardhi na majengo, ukandarasi, madini, rasilimali watu, utalii, viwanda, huduma, uchukuzi, mawasilino na miundombinu.

Send this to a friend