Rais Samia ataka wananchi kupewa elimu ya sheria zinazotungwa

0
17

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema baadhi ya sheria hususani sheria ya ardhi za kimila zinazorotesha utekelezaji wa sheria ya ardhi iliyotungwa na Serikali ambayo inamlinda mwanamke katika kumiliki ardhi.

Ameyasema hayo wakati akishiriki maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

“Kimsingi ndugu zangu, sina tatizo na sheria ya ardhi na sheria za urithi za kimila ambazo zinazingatia haki. Ila katika karne ya 21, inashangaza sana kuona mtu anasimama na anapinga mwanamke kurithi mali/ardhi aliyoiacha mume wake,” amesema.

Rais Samia azitaka TAKUKURU na ZAECA kujitafakari

Aidha, ametoa wito kwa mashirika yanahusika na masuala ya sheria kufanya tathmini na kutoa elimu kwa jamii juu ya mila na desturi zote zinazoimarisha haki na kuondokana na zile zinazodidimiza haki ya mwanamke na watoto hususani katika maeneo ya vijijini.

“Tunapotunga sheria tunaita wadau waje kutoa maoni lakini wadau wanaokuja ni wale wanaoishi Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma Arusha labda Mbeya, lakini wale wenyewe kule Watanzania wala hawana habari, wanasikia tu kwenye taarifa ya habari sheria imetungwa inasemaje ikoje hajui,”amesisitiza.

Send this to a friend