Rais Samia atangaza kuifumua na kuisuka upya Serikali

0
20

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kufanya mabadiliko kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ili kuachana na viongozi ambao wanashindwa kuendana na kasi yake.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga Mkutano wa 10 wa chama hicho ulioanza jana jijini Dodoma ambapo ameeleza kuwa wanasafari ya muda mrefu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hivyo itawapa nafasi wananchi kuona na kutathmini yaliyofanyika na wenyewe kuwa mashuhuda.

“Naomba sasa mnipe baraka zenu nikaipange Serikali pia,” amesema huku akiongeza analenga kuipanga kwa jinsi ambavyo anahisi timu hiyo itaweza kujipanga kutekeleza yale yote ambayo mkutano mkuu umepitisha.

Rais Samia: Uchaguzi CCM ukiimarishe chama kuelekea chaguzi zijazo

Ameongeza “kubwa zaidi tunapokwenda kwa wananchi, ni wananchi wenyewe wanayosema Serikali waliyofanya kwao, tofauti na utamaduni tuliokuwa nao nyuma, kwamba tunapokwenda kwa wananchi Serikali ndio tunawaambiwa tumewafanyia, wakati mwingine wanashangaa hiki kimefanyika wapi.”

Aidha katika hotuba yake, Dkt. Samia ametoa wito kwa wanachama kukijenga chama na kuepuka kujenga nyufa baina ya wanachama hasa katika kipindi cha uchaguzi ambapo makundi mengi hujitokeza na kutofautiana.

“Wakati wa uchaguzi makundi ni mengi wagombea ni wengi, tutatofautiana lakini tukimaliza tusikubali kujenga nyufa ndani ya Chama,” ameeleza.

Send this to a friend