Rais Samia atengua uamuzi wa TRA kuhusu Machinga kutumia EFD

0
38

Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga wamemsifu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na uamuzi wake wa kusitisha utaratibu uliotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwataka kuanza kutumia mashine za kielektroniki (EFD) katika kufanya malipo.

Sambamba na hilo wamemwomba Rais Dkt. Samia kuunda kikosi kazi kitachojumuisha viongozi wa wamachinga nchini, TRA, Jeshi la Polisi, viongozi kutoka halmshauri pamoja na wawakilishi wa Serikali, kukaa na kufanya upembuzi wa kuwatambua wamachinga halisi ili kuzuia wafanyabiashara wasiokuwa na sifa ya kuwa machinga kujipenyeza kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.

Viongozi wa machinga hao wamesema wamefurahishwa na maamuzi ya Rais Dkt. Samia kwa kuwa maamuzi ya awali yalifanywa kwa hila ili kuwakandamiza kwa lengo la kuwaficha watu waliojipenyeza na kujiita wamachinga wakati wao ni wafanyabiashara wakubwa.

Multichoice yaamriwa kuwalipa Simbu na wenzake TZS milioni 450

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania, Stephen Lusinde amesema lingekuwa jambo la busara endapo uamuzi wa awali uliotangazwa na TRA ungewashirika wamachinga kwa kuwa ni uamuzi unaoamua hatima yao katika ulipaji wa kodi kutokana na uwezo wao.

“Tulipaswa kufanya kazi kwa kushirikiana baina yetu na TRA, lakini cha ajabu ni kwamba wamachinga wanafanya kuitwa katika ofisi za TRA na kuulizwa mahali alipofungua biashara yake kisha kutajiwa kiasi anachotakiwa kulipa kama kodi, walitakiwa kuja kwenye biashara zetu waone biashara ya mtu ndipo wakadirie” amesema.

Chanzo: Habari Leo

Send this to a friend