Rais Samia atengua uteuzi viongozi wa juu ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu

0
55

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Frank Kanyusi Frank kuwa Kabidhi Wasii Mkuu akichukua nafasi ya Angela Anatory ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo, Frank alikuwa Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Irene Lesulie kuwa Naibu Kabidhi Wasii Mkuu akichukua nafasi ya Lina Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi Lesulie alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mashauri ya Kimataifa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Send this to a friend