Rais Samia atengua uteuzi wa bosi wa TBS

0
45

 

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Fenella Ephraim Mukangara.

Aidha, Rais ameteua Prof. Othman Chande Othman ambaye ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuchukua nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine Rais amemteua Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC) akichukua nafasi ya Prof. Humphrey P.B. Moshi aliyemaliza muda wake.

Dkt. Mlimuka ni Mkurugenzi Mstaafu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Pia, Rais amemteua Dkt. Andrew Yona Kutua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Dkt. Kutua anachukua nafasi ya Dkt. Deudatus Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.

Send this to a friend