Rais Samia atengua uteuzi wa Chalamila

0
33

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuxi wa aliyekuwa Mkoa wa Mwanza Albert Chalamila kuanzia leo Juni 11, 2021.

Kufuatia utenguzi huo amemhamisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi. Robert Luhumbi kwenda Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ally Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Batilda Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora

Aidha, Zuwena Jiri ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Buriani.

Tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadaye.

Send this to a friend