Rais Samia ateua gavana mpya wa Benki Kuu 

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Emanuel Tutuba kuwa Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Tutuba ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, Rais Samia amemteua Dkt. Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Send this to a friend