Rais Samia ateua Mkaguzi wa Ndani, Mhasibu wa serikali na Msajili wa Hazina

0
50


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 6, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

1. Amemteua Athumani Seleman Mbuttuka kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General).

Mbuttuka anachukua nafasi ya Balozi Mohamed Mtonga ambaye amestaafu na Balozi wa Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mbuttuka alikuwa Msajili wa Hazina (Treasury Registrar).

2. Amemteua Leonard John Mkude kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali (Accountant General). Mkude anachukua nafasi ya Bw. Francis M. Mwakapalila ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi, Bw. Mkude alikuwa Meneja Bajeti, Benki Kuu ya Tanzania.

3. Amemteua Mgonya A. Benedict kuwa Msajili wa Hazina. 

Benedict anachukua nafasi ya Bw. Athumani Mbuttuka ambaye ameteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Benedict alikuwa Meneja wa Masuala ya Fedha na Madeni, Benki Kuu ya Tanzania.

4. Amemteua Frank Mugeta Nyabundege kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tanzania Agriculture Development Bank). Kabla ya uteuzi huo, Nyabundege alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Oil Tanzania Limited.

5. Amemteua Casmir Kyuki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Kyuki ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Teuzi hizi zimeanza Agosti 5, 2021.

Send this to a friend