Rais Samia ateua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na viongozi wengine wanne

0
43

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji Jacob Casthom Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Jaji Mwambegele ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Semistocles Kaijage ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais amefanya uteuzi wa viongozi wengine kama ifuatavyo;

• Amemteua Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Jaji Kwariko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Jacob Casthom Mwambegele.

• Amemteua Jaji Sam Mpaya Rumanyika, Jaji wa Mahakama Kuu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

• Amemteua Prof. Khamis O. Dihenga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Prof. Dihenga anahudumu kwa Mkataba katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro. Prof. Dihenga anachukua nafasi ya Prof. William A. L. Anangisye aliyemaliza muda wake.

• Amemteua Dkt. Mussa Muhidin Kissaka, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Desemba, 2021.

Send this to a friend