Rais Samia ateua na kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya

0
41

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya Uteuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:-

1. Said Mohamed Mtanda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi amehamishiwa Wilaya ya Arusha. 

2. Abbas Juma Kayanda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu amehamishiwa Wilaya ya Moshi.

Aidha, Rais Samia amemteua Dadi Horace Kolimba, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu.

Kolimba anachukua nafasi ya Abbas Juma Kayanda ambaye amehamishiwa Wilaya ya Moshi.

Send this to a friend