Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili ambapo kwanza amteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mcha ambaye uteuzi wake ulianza Desemba 5, 2021 anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.
Kabla ya uteuzi huo, Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement), Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pili, Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.
Balozi Mushy ambaye uteuzi wake umeanza Januari 14, 2022, alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.