Rais Samia ateua viongozi wa taasisi mbalimbali

0
44

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wa taasisi mbalimbali kama ifuatavyo;

  1. Amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Dkt. Kilimbe anaendelea na wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
  2. Amemteua Bw. Hab Mkwizu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Bw. Mkwizu anaendelea na wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
  3. Amemteua Bw. Yahaya Ibrahim Mgawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti na Uvuvi Tanzania (TAFIRI).
  4. Amemteua Prof. Erick Vitus Komba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI). Prof. Komba amechukua nafasi ya Dkt. Eligy Mussa Shirima ambaye amestaafu.
  5. Amemteua Bw. Kadari Singo kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi. Bw. Singo amechukua nafasi ya Prof. Joseph Semboja ambaye amestaafu.
    Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 20 Aprili, 2021.

Aidha, Rais Samia amemteua Dkt. Natu El-Maamry Mwamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Uteuzi wa Dkt. Mwamba umeanza tarehe 19 Aprili, 2021.

Send this to a friend