Rais Samia ateua viongozi wa taasisi tatu (TIRA, JFC na EPZA)

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Baghayo Abdallah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuanzia Januari 1, 2022.

Dkt. Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).

Pia, Rais amemteua Charles Jackson Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA).

Itembe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited).

Aidha, Ernest Maduhu Mchanga ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).

Mchanga ni Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala, Tume ya pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Send this to a friend