Rais Samia ateua viongozi wawili

0
64

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Dkt. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha, Rais amemteua Dkt. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Uteuzi huo umeanza Septemba 14, 2021.

Send this to a friend