Rais Samia ateua wawili akiwa Marekani

0
36

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Yona Killagane kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO).

Pia Rais amemteua Mathew Modest Kirama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Kabla ya uteuzi huu Kirama alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma (DE), Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kirama anachukua nafasi ya Nyakimura Mathias Muhoji ambaye amestaafu.

Send this to a friend