Rais Samia ateua wenyeviti wapya TARI na NIT

0
16

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), na uteuzi huo umeanza Aprili 02, mwaka huu.

Masawe anajaza nafasi ya Dkt. Tausi Mbaga Kida ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji.

Aidha, Rais Samia amemteua Prof. Ulingeta Obadia Lebson Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Prof. Mbamba anachukua na fasi ya Prof. Blasius Bavo Nyichomba ambaye amemaliza muda wake.

Send this to a friend