Rais Samia atoa bilioni 19.6 ujenzi wa miradi ya elimu mkoani Njombe

0
123

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP mkoani Njombe.

Kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Bilioni 4.360 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya madarasa, maabara, mabweni, Bwalo la chakula jengo la utawala na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Njombe ambayo imekamilika.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Njombe, Mwalimu Nelasi Mulungu ambapo amesema pia Bilioni 1.6 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Amali ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya ya Ludewa.

Amesema serikali imetoa zaidi ya Bilioni 12.638 kwa ajili ya ujenzi wa shule 20 za kata katika mkoa huo wa Njombe.

Pia amesema serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika mkoa wa Njombe ikiwemo ujenzi wa mabweni, nyumba za walimu, na matundu ya vyoo.

Send this to a friend