Rais Samia atoa ekari 5,520 kwa vijiji 11 vya Bagamoyo na Kibaha

0
39

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ardhi ekari 5,520 kwa vijiji 11 vya Wilaya za Bagamoyo na Kibaha mkoani Pwani vinavyoizunguka Ranchi ya Taifa ya Ruvu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, David Silinde wakati wa makabidhiano ya ardhi iliyokuwa sehemu ya Ranchi ya Ruvu kwenda kwa wananchi wa wilaya hizo.

Silinde amesema Serikali kupitia Rais Samia iliunda tume shirikishi ya kitaifa mwaka 2019/2020 kutatua migogoro kwenye maeneo yake ikiwemo Ruvu kufuatia uvamizi mkubwa unaofanywa na wananchi wanaozunguka ranchi.

“Tume ilifanya kazi ya kuzunguka katika vijiji vyote 16 vinavyopakana na ranchi na kufanya uhakiki na kurudisha mipaka halisi iliyowekwa awali na kufanya tathmini ya mahitaji ya ardhi kwa wananchi ili kumaliza migogoro mipya ya uvamizi,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi walioingia kwenye mipaka mipya watoke kwa hiari yao ili kupisha shughuli za kiserikali kuendelea bila ya kuwepo kwa vikwazo na hivyo kuwa na mahusiano mazuri kati ya ranchi na wananchi.

Send this to a friend