Rais Samia atoa maelekezo kufanikisha mageuzi mashirika ya umma

0
26

Rais Samia Suluhu amesema ni muhimu Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhakikisha inasimamia ipasavyo sheria na kanuni zilizopo ikiwemo kusimamia ipasavvyo utekelezaji wa mikataba ya utendaji kazi (performance contract) katika kuhakikisha kuwa taasisi na mashirika ya umma yanajiendesha kwa tija na kupunguza gharama za uendeshaji kutoka serikalini.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma mkoani Arusha ambapo ameiagiza Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kushirikiana na Wizara za kisekta kuanza mchakato wa kisera na kisheria kukamilisha utekelezaji wa mabadiliko katika taasisi za umma kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

“Hakikisheni mnafuata utaratibu na ushirikishwaji wa wadau wanaohusika, moja ya hatua ya kuzingatia ni kuwa asiwepo mtumishi atakayepoteza kazi na stahiki zake, na kwamba mali za umma zilindwe kikamilifu katika kipindi cha mpito,” amesema.

Rais Samia: Mabalozi fanyeni kazi kwa matokeo msisubiri matukio

Aidha, Rais Samia amesema Serikali iko kwenye mchakato wa kutunga sheria itakayobadilisha hadhi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma, pia inaangalia uwezekano wa kuanzishwa kwa mfuko wa uwekezaji wa umma ili kuondoa utegemezi kutoka kwenye mfuko mkuu wa Serikali.

Mbali na hayo, amewataka wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma kufanya kazi kwa ufanisi kwa kusimamia vyema taasisi hizo, na kuwaagiza wote wanaosuasua katika utendaji wao kuchukua hatua za haraka.

“Msinilazimishe kupangua, pangua pangua sio jambo ninalolipenda, na mkiniona nimepangua mjue imenibidi nifanye hivyo, kwahiyo kwa wale ambao hawawezi

Send this to a friend