
Katika kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 1548, ambapo wafungwa 22 kati yao wanaachiliwa huru tarehe 9 Disemba, 2024, na wafungwa 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.