Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 376

0
40

Katika kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 376 walioko magerezani ambapo wafungwa sita wataachiwa huru leo na wengine 370 watabaki kumalizia sehemu ya vifungo vilivyobaki baada ya kupewa msamaha.

Wafungwa waliopata msamaha huo sharti wawe wamehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka mitatu, ambao wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia gerezani kabla ya Februari 26, 2023, wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wadogo wanaonyonya na wasionyonya.

Rais Samia atengua uteuzi na kuvunja Shirika la Reli

Aidha, wafungwa wasiohusishwa na msamaha huo ni pamoja na waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa, waliojaribu kujiua na kuua watoto wachanga, wafungwa wanaotumikia vifungo vya nje, waliopatikana na hatia ya kuhujumu uchumi, na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu/wizi, utakatishaji wa fedha, rushwa na madawa ya kulevya.

Pia waliohukumiwa kwa makosa ya kujamiiana, utekaji na wizi wa watoto, kuwapa mimba wanafunzi, waliokutwa na viongo vya binadamu, unyang’anyi wa kutumia silaha, kumiliki silaha, risasi, milipuko au kujaribu kutenda makosa hayo.

Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya ujangili au kupatikana na nyara za Serikali, waliotoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi au kusaidia kutenda makosa hayo, wafungwa warudiaji na waliowahi kupoata msamaha wa Rais na wafungwa wa madeni (cicil pisoners).

Send this to a friend