Rais Samia atuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amemtuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Amani mkoa wa Mjini Magharibi, Mussa Hassan Mussa (63) kilichotokea leo Oktoba 13, 2022 Zanzibar.

Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mbunge huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika utumishi wa umma.

Aidha, amemtaka Spika wa Bunge kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huo.

Send this to a friend