Rais Samia awafuta machozi wananchi wa Ukerewe

0
47

Wizara ya Afya imesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuona changamoto wanayopitia wananchi wa Ukerewe ya kukosa huduma bora za afya kwa muda mrefu, ametenga ekari 16 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali yenye hadhi ya Mkoa itakayosogeza karibu upatikanaji wa huduma bora za afya.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo mara baada ya kukagua eneo la ekari 16 ambapo patajengwa hospitali yenye hadhi ya mkoa.

“Baada ya Mheshimiwa Rais kusikia kilio cha Wana-Ukerewe amefanya maamuzi bora ya kuwaletea hospitali hii ambayo itakuwa ni ghorofa mbili, hii haijawahi kutokea kwa sababu ya mapenzi yake kwenu,” amesema.

Ameongeza kuwa “Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe ambayo ilitarajiwa kuwa ya Mkoa kwa sasa itaendelea kuwa Hospitali ya Wilaya ambapo Hospitali ya Mkoa itajengwa Katika Kata ya Bulamba kijiji hiki cha Bukindo.”

Rais Samia atoa ekari 5,520 kwa vijiji 11 vya Bagamoyo na Kibaha

Aidha, amesema kwa kushirikiana na wataalam wake ameridhishwa na eneo hilo na sasa hatua ya uchoraji wa ramani unaanza ili kuwezesha kujua thamani ya ujenzi huo ambapo ujenzi wa hospitali hiyo unatarajia kuanza mapema iwezekanavyo.

“Hospitali hii itakayojengwa hapa itakuwa chachu katika utoaji wa huduma bora za afya ikiwemo za upasuaji, magonjwa ya wanawake na uzazi pamoja na utolewaji wa huduma za magonjwa ya watoto.” ameongeza.

Send this to a friend