Rais Samia awaongezea muda wa miaka 15 wakazi wa Magomeni Kota

0
55

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwaongezea muda wa ununuzi wa nyumba wakazi 644 wa Magomeni Kota hadi miaka 30 ikijumuisha miaka mitano ya kukaa bure.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kondoro amesema baada ya wakazi wa Magomeni Kota kujulishwa juu ya gharama wanazopaswa kulipia ambazo ni TZS milioni 48.5 kwa nyumba ya chumba kimoja na TZS milioni 56.8 kwa nyumba ya vyumba viwili walimwomba Rais Samia kuwapunguzia gharama na kuongeza muda wa kulipa.

“Baada ya kupokea maombi hayo, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwaongezea muda wa ununuzi wakazi wa Magomeni Kota kutoka miaka 15 iliyoelekezwa awali hadi miaka 30 ikijumuisha miaka mitano ya kukaa bure,” amesema.

Kondoro ameongeza kuwa baada ya kuwajulisha wakazi 644 kwa barua, TBA iko tayari kuwatambua walio tayari kutekeleza utaratibu huo wa ulipaji na kuingia nao mkataba wa mkazi mnunuzi ndani ya siku 14.

Aidha, amesema TBA iko tayari kuwatambua wakazi wasiokuwa tayari kutekeleza utaratibu huo, kwani wataruhusiwa kukaa bure kwa miaka mitano, na baada ya muda huo kutimia watazirejesha nyumba hizo kwa wakala.

Send this to a friend