Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kuacha kutumia vibaya fedha zinazotolewa katika wilaya kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kuwaapisha viongozi wateule iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam na kuwataka viongozi kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupata imani ya wananchi badala ya kustareheka na marafiki na kusahau wajibu wao kama viongozi.
Maagizo 9 ya Makamu wa Rais ufunguzi wa Nane Nane
“Kuna fedha inakuja mnakaa nayo kwenye akaunti, fedha haitumiki, ukiuliza kuna nini, mvutano. Hiyo fedha imeletwa kwenu siyo kwamba haina matumizi huku Serikali kuu, kuna matumizi makubwa sana, tumeamua kuhudumia wananchi” amesema.
Aidha, amesema wakuu wa mikoa wote wamebadilishwa kwa lengo la kuongeza nguvu katika utendaji wao pasipo kuwepo na upendeleo wowote kwa viongozi hao.
“Ninapofanya teuzi siangalii kabila la mtu, siangalii rangi ya mtu, anakotoka mtu, siangalii chochote. Naangalia sifa, uwezo, uaminifu wake kwa nchi na Serikali,” amesema.