Rais Samia awapa wananchi rungu dhidi ya viongozi wazembe

0
42

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuzungumza pindi wakuu wa Mikoa na wilaya pamoja na viongozi wengine wanaposhindwa kufanya kazi yao vizuri.

Rais ameyazungumza hayo alipokuwa Lamadi Mkoani Simiyu akielekea Mkoani Mara
kwenye maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Kama kuna Mkuu wa Mkoa anatetereka, Mkuu wa wilaya au viongozi wengine tuambieni, tumewaleta watumikie watu, tutaleta wengine tunao wengi kwenye akiba” amesema.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amewasilisha ombi la wakazi wa mji mdogo wa Lamadi wilaya ya Busega kuhusu kukosekana kwa stendi na soko, hali inayowafanya kupata taabu katika shughuli zao za kila siku.

Rais amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Simiyu kusimamia fedha zilizotelewa
na serikali kikamilifu ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa. Pia amewaahidi wananchi wa Simiyu
stendi mpya na soko kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo litakalotumika saa 24

Rais Samia atakuwa katika ziara ya siku nne Mkoani Mara ambapo atahudhuria maadhimisho ya miaka 45 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Musoma.

Pia atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta za Afya, maji na utawala yenye thamani ya zaidi ya TZS bilioni 126.21.

Send this to a friend