Rais Samia awapangia vituo mabalozi wawili, mmoja ahamishwa

0
51

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wafuatao:

1. Balozi Anisa Kapufi Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

2. Balozi Innocent Eugene Shio, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Utawala Fedha na Mipango, Chuo cha Diplomasia-Dar es Salaam kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Aidha, Rais Samia pia amemhamisha kituo cha kazi Balozi Baraka Haran Luvanda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Kabla ya uhamisho huo Balozi Luvanda alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Send this to a friend