Rais Samia awasihi wananchi kuiga mazuri ya Membe

0
49

Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba Watanzania kuiga mazuri yote yaliyofanywa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Hayati Bernard Membe pamoja na kumuombea.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Samia aliyemwakilisha katika mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika leo katika kijiji cha cha Chiponda, Rondo mkoani Lindi.

“Watanzania, wananchi wa Lindi na hapa Rondo, Mheshimiwa Rais Samia amewataka mmuenzi yale yote mema aliyotenda Membe wakati wa uhai wake lakini pia endeleeni kumuombea ili mwenyezi Mungu amlaze mahali pema,” amesema

Akiongea kwa niaba yake, amesema kifo cha Membe kimewaacha Watanzania na wana-Lindi na butwaa kubwa, huzuni pamoja na simanzi, na kutoa pole kwa wote walioguswa na msiba ndani na nje ya nchi.

Send this to a friend