Rais Samia awataka viongozi kutokuwa waoga wa kufikiri

0
26

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kutoogopa kufanya maamuzi yenye nia njema kwa manufaa ya nchi.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 14, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akihutubia mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni akiwemo Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo ambapo amebainisha kuwa ili Tanzania iendelee ni lazima kupanga na kufikiri.

“Na mie niwaombe msiende kuona uoga katika kufikiri wala kuja na mapendekezo ambayo nyie mnaona yanaweza kuiendesha Tanzania vizuri. Kwa sababu kwenu ni kuwaza na kutuletea kisha vyombo mbalimbali vitakaa na kufikiri,” ameeleza.

Akizungumzia kuhusu suala la fursa, Rais Samia amesema wakati taifa likiendelea kulumbana kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam, nchi jirani wao wanaomba kupata fursa hiyo ya kupata uwekezaji katika bandari zao, hivyo ni vizuri kuona fursa zinavyoweza kuja na kuondoka kwa haraka iwapo hazijatumiwa.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amempongeza Rais Samia kwa kuirejesha Tume ya Mipango na kuiweka chini ya Ofisi ya Rais, na kubainisha kuwa tume hiyo  ni chombo muhimu kwani maendeleo endelevu ya Taifa yanatokana na mipango inayaandaliwa na Tume hiyo.

Send this to a friend