Rais Samia awataka viongozi kutotumia vyeo kunyanyasa watu

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan amesema mabadiliko aliyoyafanya ya viongozi mbalimbali Serikalini si adhabu kwa viongozi hao, bali yanalenga kuimarisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Rais amesema kauli hiyo leo Septemba 01, 2023 alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali wateule wakiwemo mawaziri na manaibu pamoja na makatibu wakuu katika Ikulu Ndogo, Zanzibar.

“Nataka nisisitize kwamba, mabadiliko haya si adhabu ni mabadiliko ya kawaida ya kuimarisha maeneo yetu. Ninachotarajia kwenu ni commitment [kujitoa] kwenye kazi zenu, utumishi,” amesema.

Aidha, amewataka viongozi kutotumia vyeo walivyonavyo kuwanyanyasa watu na kuonyesha majivuno, badala yake wawatumikie wananchi kwa upole, maarifa na uadilifu mkubwa ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili taifa.

Majibu ya Katiba kuhusu uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu

“Tunachotaka ni mabadiliko tunayoahidi watu, tunaahidi mambo mengi, twendeni tubadilikeni, amesisitiza Rais Samia.

Kwa upande wa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewasihi viongozi walioapishwa kusikiliza kero za wananchi wa pande zote mbili wa Bara na Zanzibar na kuzifanyia kazi, akitolea mfano katika sekta ya Ardhi na Maliasili ambapo kuna migogoro inayoendelea kwenye jamii.

Send this to a friend