Rais Samia awataka wanajeshi wanaoteuliwa uraiani kutokuvaa kombati za jeshi

0
87

Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza Makanali walioapishwa kuwa wakuu wa mikoa kuacha kuvaa kombati katika majukumu yao ya kazi mpaka pale watakaporejea jeshini.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule leo Agosti 1, 2022 Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Rais Samia awaonya viongozi matumizi mabaya ya fedha za Serikali

Makanali walioapishwa ni Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Kanali Laban Elias Thomas aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

“Makanali hatuwatarajii kuvaa kombati mkiwa Wakuu wa Mikoa, kwahiyo kombati zipumzike mpaka mtakaporudi jeshini.” amesisitiza Rais Samia Suluhu.

Hata hivyo amewashukuru viongozi waliotolewa kwenye nafasi zao kwa sababu mbalimbali na kusema kuwa wamechangia taifa kwa kipindi ambacho walikuwa wakihudumu nafasi hizo.