Rais Samia: Haki itapunguza mlundikano wa mahabusu gerezani

0
36

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka mawakili kusimamia sekta ya sheria kwa uadilifu na kwa uaminifu ikiwa ni pamoja na kutenda haki ili kupunguza mlundikano wa mahabusu magerezani.

Ameyasema hayo leo Septemba 29, Jijini Dodoma wakati akishiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

“Ninyi ni mainjinia wa kucheza na vifungu vya sheria, anaweza kabisa mtu ana kosa mkaenda mkacheza na vifungu vya sheria na mkashindana kitaaluma mkataka kuonyeshana, mkamtoa mwenye kosa mkasema hana kosa, na yule ambaye ana kosa mkasema hana kosa, sasa engineering hiyo haiwapeleki pazuri, fanyeni engineering ya sheria inayowasimamisha kwenye haki,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, ametoa wito kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na mawakili wote wa Serikali kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu kwa umma hususani sheria zinazowagusa zaidi wananchi na taratibu za namna ya kupata haki zao ili kupunguza mlundikano wa mashauri ambayo hayana ulazima wa kufikishwa mahakamani kwaajili ya utatuzi.

Mbali na hayo amemshauri Mwanasheria Mkuu kuwepo kwa mafunzo ya mara kwa mara kwa mawakili kwakuwa utaalam wa sheria hubadilika kila mara pamoja na kutojisahau kwa mawakili katika maeneo yao ya kazi.

Send this to a friend