Rais Samia: Hakuna mwenye ubavu wa kuligawa au kuliuza Taifa hili

0
22

Kufuatia maneno yanayoendelea kuzungumzwa kuhusu mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai, Rais Samia Suluhu Hassan amewatoa hofu Watanzania na kusisitiza kwamba hakuna mtu mwenye ubavu wa kuligawa, kuliuza taifa au kuharibu amani ya nchi iliyojengwa kwa muda mrefu.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mkoani Arusha, Rais Samia amesema aliamua kutotia neno katika sakata la uwekezaji wa bandari na ataendelea kufanya hivyo, lakini akiwahakikishia Watanzania kuwa taifa liko katika hali ya usalama.

“Niliamua kunyazama kimya na naendelea kunyamaza kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye taifa hili,” amesema.

Aidha, Rais amesema Serikali inaendelea kuimarisha misingi ya utawala bora kwa kufuata misingi ya sheria, demokrasia na maadili ya Watanzania kwa kutumia falsafa ya 4R ambayo ni maridhiano, kustahimiliana, mabadiliko na kujenga upya taifa.

Mtoto Hamimu aliyekuwa na matatizo ya ngozi akabidhiwa nyumba na Rais Samia

Naye Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo ameiomba Serikali kukemea kwa nguvu wale wote wanaoonesha dalili yoyote ya kuligawa taifa kwa kutumia dini au siasa hata kama ametoa hoja ya kuipendeza Serikali lakini yenye misingi isiyofaa kwa taifa.

“Niombe Serikali yako kukataa na kukemea kwa nguvu yote wale wote wanaoonesha dalili za kutugawa kwa utofauti wa dini zetu, hata pale mtu anaposema jambo la kuipendeza Serikali iwapo amejenga hoja yake katika msingi.

Send this to a friend