Rais Samia: Jamii inapaswa kuwarithisha watoto mila na desturi zetu

0
14

Rais Samia Suluhu Hassan amesema jamii inapaswa kuhakikisha watoto wanafundishwa na kukua katika maadili mema ili kuwa na taifa lenye maadili na nidhamu.

Akizungumza Agosti 31, 2023 wakati kilele cha Tamasha la Kizimkazi, Paje visiwani Zanzibar, amesema iwapo jamii inataka kulinda mila na desturi zake, haina budi kuhakikisha tamaduni na mila hizo zinarithishwa kwa watoto.

Aidha, Rais Samia amesema katika Tamasha hilo mambo kadhaa yamezingatiwa ambayo ni vema yakirithishwa kwa watoto ikiwemo lugha ya Kiswahili, vyakula vya asili, kazi za kiuchumi pamoja na utamaduni wa ngoma za asili.

Baadhi ya miradi iliyozinduliwa na Rais Samia katika sherehe za Kizimkazi kwa upande wa sekta ya elimu ni pamoja na Skuli ya Kizimkazi, madarasa 11 yaliyofanyiwa marekebisho na TASAF, ukarabati wa madarasa sita yaliyofanyiwa ukarabati katika kijiiji cha Muyuni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika shule ya Tasan Makunduchi.

Kwa upande wa utalii, Rais Samia amezindua hoteli kubwa ya nyota tano iitwayo Kwanza Resort ambayo inaajira zaidi ya vijana 300 pamoja na kuzindua mradi wa maji ambao umesaidia kuondoa tatizo la maji kijijini hapo.

“Tumezindua mradi wa maji ambao kwa miaka kadhaa kijiji cha Kizimkazi eneo lote lilikuwa na matatizo ya maji, kwa kushirikiana na ZAWA na DAWASA tumeweza kuondosha tatizo la maji, DAWASA wameleta utaalam tumeondoa tatizo la maji na bado mradi unaendelea,” ameeleza.

Send this to a friend