Rais Samia: Kama mtu amevunja sheria ashughulikiwe haraka

0
43

Rais Samia Suluhu Hassana ametoa msisitizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za kisheria haraka iwezekanavyo kwa mtu au kikundi chochote kinachovunja sheria za nchi kwa kisingizio chochote.

Ameyasema hayo leo Septemba 04, 2023 katika ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Waandamizi pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika Oysterbay Polisi jijini Dar es Salaaam.

“Kama wanavunja sheria ya nchi huyo amevunja sheria za nchi na lazima ashughulikiwe kama mvunjaji wa sheria za nchi,” amesisitiza Rais Samia.

Aidha, amesema Serikali inakwenda kuangalia namna itakayokuwa bora kwa kila sekta na ambayo haitaleta athari mbaya kwa mifuko ya Serikali katika suala zima la kikokotoo kwa wastaafu ili kuepusha malalamiko mengi ambayo yanaendelea.

“Masuala ya vikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo hapana, ni hali ya kiuchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo, tukisema kila anayetoka bumu lako hili hapo miaka miwili tu mifuko ile imekakuka.

Kwahiyo tuliweka hii ili kuweka sustainability [uendelevu] ya mifuko, sasa kwa sababu kimepigiwa kelele sana sio tu na Jeshi la Polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia tuone njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi,” amesema.

Mbali na hayo, Rais Samia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa katika hali ya utulivu na usalama pamoja na kuwataka viongozi wake kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maadili ili na wengine wafuate.

Send this to a friend