Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa

0
47

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kugharamia matibabu ya Edgar Mwakabela maarufu ‘Sativa’ aliyetekwa, kujeruhiwa na kutelekezwa msituni Katavi, kuanzia sasa anapoendelea kupatiwa huduma hadi atakapopona pamoja na kuhakikisha uchunguzi wa tukio hilo unafanyika.

Hayo ameyasema Kiongozi Mstaafu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya kuzungumza na Rais Samia juu ya tukio la kutekwa kwa kijana huyo pamoja na matukio mengine ya watu kupotea katika siku za hivi karibuni.

“Nimemsihi ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama juu ya tukio hili pamoja na na mengine ya namna hii.

Kama taifa tunahitaji kushirikiana pamoja na kukomesha mambo ya watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni. Yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili,” amesema.