Rais Samia kuhudhuria Mjadala wa Kilimo Marekani

0
50

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Des Moines, Lowa nchini Marekani kuhudhuria Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug ulioandaliwa na Taasisi ya World Food Prize Foundation ya nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia ni miongoni mwa Marais wanne kutoka Afrika waliopewa heshima ya kushiriki na kuchangia mjadala huo unaohudhuriwa na viongozi, wataalamu, watu mashuhuri, watunga sera hususani za kilimo, lishe na usimamizi wa rasilimali.

Lengo la majadiliano hayo imeelezwa kuwa ni kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula duniani ambayo inachochewa na mabadiliko ya tabianchi.

Mbali na Mjadala huo, Rais Samia atashiriki hafla ya utoaji tuzo ya World Food Prize 2024 kwa watu wenye mchango mkubwa katika sekta ya kilimo, ikiwa ni mwendelezo wa kumuenzi Hayati Dkt. Norman E. Borlaug ambaye alikuwa akihamasisha usalama wa chakula duniani.

Aidha, Rais Samia atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi kutoka Serikali na sekta binafsi ya nchini Marekani hususani waliopo kwenye sekta ya kilimo kwa lengo la kujadili uwekezaji katika sekta hiyo na kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta hiyo ambayo.

Send this to a friend