Rais Samia kununua kila goli la Simba na Yanga kwa TZS milioni 5

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kununua kila bao litakalofungwa na klabu za Simba na Yanga katika michezo yao ya kimataifa ya mwisho wa wiki hii kwa shilingi milioni 5 .

Hayo yamesemwa Februari 14, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati timu hizo mbili zikisubiri mechi ya pili ya hatua ya makundi baada ya kufungwa mechi zao za kwanza wakiwa ugenini.

Klabu ya Simba itacheza Jumamosi Februari 18, 2023 saa 1:00 jioni dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Klabu ya Yanga ikitarajia kuikaribisha TP Mazembe Jumapili Februari 19, 2023 saa 1:00 jioni katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, zote zikiwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Send this to a friend