Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo.
Akiwa nchini Ghana, Rais Samia anatarajia kushiriki mdahalo wa wakuu wa Nchi za Afrika utakaoangazia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa bei ya vyakula na matumizi ya nishati endelevu.
Aidha, Rais Samia anatarajia kupokea Tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa Nchi iliyofanya vizuri zaidi.
Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka katika Mkutano wa AfDB ambao kwa mwaka 2022 unafanyika Accra, Ghana.