Rais Samia kuongoza Wafanyabiashara maonesho ya Biashara Dubai (Expo 2020 Dubai)

0
41

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika kutangaza vivutio vya utalii na fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo nchini katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dubai (Expo 2020 Dubai).

Rais Samia ataongoza ujumbe huo Februari 26, 2022, siku iliyotengwa kwa ajili ya Tanzania kuonesha bidhaa na fursa mbalimbali katika maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 2021 na kutarajiwa kufikia ukomo Machi 2022.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dotto James amesema ni fahari kwa Tanzania kupata fursa kwenye maonesho hayo makubwa dunaini ambayo yanafanyika kwa kipindi cha miezi sita, na hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Manesho hayo yanahusisha mataifa 191 duniani kote na Tanzania imekuwa ikishiriki tangu mwaka 1971.

Send this to a friend