Rais Samia kushiriki mkutano wa pamoja kati ya Afrika Kusini na Tanzania

0
46

 

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya Kiserikali nchini Afrika Kusini Machi 16, mwaka huu kwa mwaliko maalum kutoka kwa Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.

Katika ziara hiyo ya kiserikali Rais Samia atashiriki katika mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushrikiano wa kitaifa kati ya Afrika Kusini na Tanzania (BNC) wenye lengo la kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.

Kongamano hilo la biashara litafanyika chini ya kaulimbiu “Kuanzisha Makubaliano Mapya kati ya Afrika Kusini na Tanzania Kuelekea Viwango vya Juu vya Biashara na Uwekezaji.”

Nchi 10 Afrika zinazodaiwa zaidi na China

Aidha, kongamano hilo litaangazia kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, mafuta na gesi, madini na maendeleo ya miundombinu ambapo  Rais Ramaphosa na Rais Samia wakitarajiwa kuhutubia kikao cha mawasilisho cha jukwaa hilo.

Tanzania ni miongoni mwa washirika wakubwa wa kibiashara wa Afrika Kusini ambapo jumla ya biashara kati ya Afrika Kusini na Tanzania iliongezeka kutoka TZS bilioni 891.5 mwaka 2021 hadi TZS trilioni 1.1 mwaka 2022.

Uhusiano huo mkubwa wa kiuchumi unathibitishwa na uwepo wa zaidi ya makampuni 250 ya Afrika Kusini katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Send this to a friend