Rais Samia kuwagharamia walioshindwa kupandikiza figo

0
80

Wagonjwa wenye changamoto ya figo wanaohitaji kupandikizwa figo ambayo ni tiba stahiki kwa wagonjwa wanaosafisha damu na hawana uwezo wa kulipia gharama za upandikizaji watahudumiwa kupitia fedha alizotoa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili ziweze kufanya kazi hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wachangia viungo duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 13 na kuhudhuriwa na wananchi waliopandikizwa figo pamoja na wenzao waliowachangia figo.

Prof. Janabi amesema kwa sasa wanatafuta seti ya wagonjwa 10 na ndugu zao 10 ambao wapo tayari kuwachangia figo na watakapokidhi vigezo husika watanufaika na huduma hiyo.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazopandikiza figo barani Afrika ambapo katika kipindi cha miaka saba tangu kuanzishwa huduma hiyo nchini, wagonjwa 102 wameishapandikizwa kupitia kampasi mbili za Upanga na Mloganzila.

Send this to a friend