Rais Samia kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Mnara wa Mashujaa

0
42

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mnara wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadalizi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatakayofanyika kesho Julai 25 jijini Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Kikwete: Niliuona uwezo wa Rais Samia kiuongozi tangu 2001

Waziri Jenista amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika mikoa na wilaya zote nchini kwa kufanya shughuli za kijamii kama kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira ya kijamii na kuadhimisha kumbukumbu ya Mashujaa kwa mikoa na wilaya ambayo ina minara au makaburi ya mashujaa.

“Katika kukuza uzalendo kwa wananchi nchini, maadhimisho haya ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Mwaka huu 2023, yatafanyika katika uwanja huu kwa mara ya kwanza ikiwa ni agizo la Rais ambapo aliagiza kujengwa kwa mnara wenye hadhi ya makao makuu ya nchi, hatua inayoonesha nia njema ya Mheshimiwa Rais anavyojali, kuithamini na kuilinda hazina ya historia ya nchi yetu,” amesema.

Send this to a friend