Rais Samia kuzindua kiwanda cha nne kwa ukubwa Afrika

0
38

Rais Samia Suluhu Hassan kesho Desemba 3, 2021 anatarajiwa kuzindua kiwanda kipya, Raddy Fibre Manufacturing, kilichopo wilayani Mkuranga, Pwani kinachotengeneza nyaya za mawasiliano kwa ajili ya mkongo wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge amesema kiwanda hicho ni cha nne kwa ukubwa Afrika na kwamba kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa Mkuranga na Taifa, na chachu ya kukuza uchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo sambamba na kukuza teknolojia ya mawasiliano.

Kukamilika kwa kiwanda hicho kutatoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira na biashara kama vile mamalishe ambao watawahudumia wafanyakazi wa kiwanda.

Kunenge ameongeza kwamba katika ziara yake Mkuranga, Rais atasimama na kuzungumza na wananchi wa eneo la Vikundi, na amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumpokea.

Send this to a friend