Rais Samia mgeni rasmi siku ya Mashujaa

0
41

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, itakayofanyika kitaifa Julai 25, mwaka huu mkoani Dodoma.

Amesema hayo leo baada ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo, katika viwanja vya Mashujaa mkoani humo na kuweka wazi kuridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na kamati ya maadhimisho kitaifa kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

“Sherehe hii itafanyika kitaifa mkoani Dodoma na itaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, viongozi wastaafu na viongozi wengine wa kitaifa.” amesema.

Watanzania wengi hatarini kuwa vipofu

Amesema, Rais Samia aliridhia maadhimisho hayo yafanyike kitaifa mkoani Dodoma, lakini pia akaelekeza yafanyike nchi nzima kwa wakuu wa mikoa kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kwenye maeneo muhimu ya kumbukumbu katika mikoa yao.

Send this to a friend