Rais Samia: Mnajigawa mafungu, mnapambana kwa ajili gani?

0
44

Rais Samia Suluhu Hassan amevisihi vyama vya siasa kuacha kupambana na Serikali na badala yake kushirikiana kufanya kazi ili kuijenga Tanzania.

Ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) katika ukumbi wa PSSSF jijini Dar es salaam.

“Niliwaambia wenzenu wa vyama vya siasa, tunapambana kwa kitu gani? Sisi sote tunaendesha siasa za Tanzania, wote lengo letu ni kujenga Tanzania, mnajigawa mafungu, mnapambana kwa ajili gani?” amesema Rais Samia

Aidha, katika hotuba yake, Rais Samia ameutaka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kutoa elimu kwa umma waijue katiba yao, ili wakati wanapodai haki, wajue pia na wajibu wao.

Send this to a friend