Rais Samia: Msiseme kwamba mama anazunguka sana

0
39

Rais Samia Suluhu Hassan amesemakwamba ziara zote anazofanya zinalenga kufungua fursa mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza na wakazi wa Arusha leo ameesema si sahihi wananchi kusema kwamba anazunguka sana, kwani hafanyi hivyo kwa maslahi binafsi, bali kwa manufaa mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Tukizunguka hivi, msiseme ‘mama anazunguka tu,’ sitazunguka bila sababu. Nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi duniani, sasa hivi kazi ni moja tu, ni kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania,” Rais Samia.

Tangu aingie madarakani Machi 19 mwaka huu, Rais Samia amefanya ziara katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda na Rwanda.

Miongoni mwa mamufaa ya ziara yake ni pamoja na kumalizw kwa mgogoro wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kusainikiw kwa mikataba y utekeleza wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Aidha, ametumia jukwaa hilo kueleza mipango ya serikali yale kukabiliana na tatizo la ajira hasa kwwa vijana na kuweka wazi kwamba serikali itajenga chuo cha TEHAMA kwa ajili ya mafunzo, itajenga maeneo yenye huduma mbalimbali ili vijana wayatumie kufanya kazi, na itaendelea kutoa mikopo kw wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu.

Send this to a friend