Rais Samia: Msiwabughudhi wananchi mnapowaomba michango

0
17

Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya viongozi wa Halmashauri ya Makete kuacha kuwabughudhi wananchi pindi watakapowafuata kuomba michango ya taa za barabarani bali wachange kwa nafasi zao na siyo amri.

Aizungumza na wananchi mara baada ya kupokea taarifa ya mradi wa barabara ya Njombe hadi Moronga (107.4km), Rais Samia ameomba viongozi kutafuta pesa kwa njia ya kistaarabu na siyo kuwabughudhi wananchi.

“Wananchi wametaka taa, wamekubali tuchange, Serikali 100 na wenyewe 100. Lakini najua Halmashauri mnafedha za maendeleo, megeni huko angalieni mmepata ngapi huko, kitakachobaki mzitafute kwa njia nyingine.” amesema.

Rais Samia awaonya viongozi matumizi mabaya ya fedha za Serikali

Aidha, amewasihi wananchi wa Makete kutunza miundombinu inayotengenezwa na Serikali kwa faida yao wenyewe kwa kuwa inapoharibiwa inachukua muda mrefu kwa Serikali kurudi na kuitengeza tena.

Rais Samia amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kuendesha kuuboresha mji huo kwa miundombinu bora ya barabara pamoja na kutegemea wageni wengi watakaokwena kuutembelea mji huo kutokana na hali ya hewa iliyopo mkoani humo.

Send this to a friend