Rais Samia: Nchi za jirani zinatamani fursa tuliyoipata

0
42

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesisitiza kuwa wakati Tanzania inaendelea kujadili makubaliano ya bandari na kampuni kubwa ya Dubai, bandari pinzani katika ukanda huo zinaweza kuchangamkia fursa hiyo.

Akitoa kauli yake kwa mara ya kwanza hadharani leo kuhusu suala hilo katika hafla ya uapisho wa viongozi jijini Dar es Salaam, Rais Samia ametoa onyo kwamba fursa huja na kwenda haraka kwa wale ambao hawana uamuzi wa kuchukua hatua wakati huo.

Rais Samia hakutaja majina yoyote, lakini muungano wa kisiasa nchini Kenya, ambao ulipinga mazungumzo kati ya serikali ya Uhuru Kenyatta na DP World mwaka 2022, kwasasa unatafuta nafasi kukodisha bandari za Kenya kwa DP World na wafanyabiashara wengine wa kimataifa.

Kenya inaweza kutumia fursa ya kucheleweshwa kwa mazungumzo kati ya DP World na Tanzania kuvutia mwendeshaji wa bandari wa kimataifa kwenda bandari za Mombasa au Lamu.

Send this to a friend